Kipa wa Manchester United, David de Gea alifikiria kuihama timu hiyo kufuatia kushutumiwa tangu ajiunge nayo kwa kitita cha paundi milioni 18 akitokea Atletico Madrid mnamo mwaka 2011.
Mhispania
huyo alilaumiwa kwa magoli ya mwaka 2011 katika mchezo wa ngao ya Hisani dhidi
ya Manchester City, na pia kwa makosa yake dhidi ya Basle na Benfica yaliyoipelekea
Manchester United kufunga virago mapema katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya
katika msimu huo.
Hata hivyo
De Gea, ambaye sasa amecheza zaidi ya mechi 130 akiwa na Manchester United,
amesema alifanikiwa kupita kwenye kipindi kigumu mno jambo lililochangia yeye
kuboresha kiwango chake.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni