Uchunguzi
unaendelea katika hospitali moja huko Madrid baada ya muuguzi Mhispania kuwa
raia wa kwanza wa nchi hiyo kubainika kuwa na virusi vya ugonjwa hatari wa
Ebola akiwa nchini mwake.
Muuguzi
huyo alihusika katika kumtibu daktari Mmishonari ambaye alikufa kwa ugonjwa huo
baada ya kusafirishwa kwa ndege hadi Hispania akitokea Afika Magharibi kwa ajili ya kupatiwa
matibabu.
Tume ya Ulaya
imeitaka Hispania kuelezea ni kwa jinsi gani muuguzi huyo aliweza kuambukizwa
virusi vya Ebola.
Ugonjwa wa Ebola umeshaua watu 3,400 tangu
kutokea mlipuko wake wengi wao wakiwa ni kutoka nchi za Afrika Magharibi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni