Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar
Pistorius anarejea mahakamani baadae leo baada ya kutiwa hatiani kwa
kumuua mpenzi wake mwanamitindo Reeva Steenkamp.
Pistorius amekutwa na hatia ya
kumuua bila ya kukusudia Steenkamp mwezi uliopita na mahakama
kumfutia uwezekano wa kosa la kuua kwa makusudi.
Jaji Thokozile Masipa anatarajiwa
kusoma adhabu itakayomkabili Pistorius baada ya siku kadhaa za
malumbano ya kisheria na ushahidi.
Pistorius anakabiliwa na kifungo
jela cha miaka 15, ingawa Jaji Masipa anaweza kutotoa adhabu hiyo na
badala yake amtake alipe faini.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni