.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 9 Oktoba 2014

KAMPUNI YA DAVIS & SHIRTLIFF YATOA MSAADA WA MTAMBO WA KUSAFISHA MAJI KUWA SAFI NA SALAMA KWA MAHABUSU YA WATOTO ILIYOPO UPANGA JIJINI DAR ES SALAAM LEO


Mgeni rasmi ambae pia ni Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Mh Dunford Makalla akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mtambo wa kusafisha maji uliotolewa na Kampuni ya DAVIS & SHIRTLIFF kwa Mahabusu ya watoto iliyopo Upanga Jijini Dar Es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya DAVIS & SHIRTLIFF. Bw Benjamin Munyao.

Mgeni Rasmi ambae pia Ni Kamishna wa Ustawi wa Jamii, Mh Dunford Makalla akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Mtambo wa Kusafisha maji kuwa safi na salama kwaajili ya kunywa uliotolewa na Kampuni ya DAVIS & SHIRTLIFF katika mahabusu ya watoto iliyopo upanga Jijini Dar Es Salaam leo.


Kaimu Afisa Mfawidhi wa Mahabusu ya Watoto iliyopo Upanga Bi Zuhura Mfinanga akisoma risala fupi kwa Mgeni rasmi kabla ya Makabidhiano ya Mtambo wa kusafisha maji kuwa safi na salama kwaajili ya kunywa uliotolewa na kampuni ya DAVIS & SHIRTLIFF.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya DAVIS & SHIRTLIFF, Bw Benjamin Munyao akisoma maelezo mafupi juu ya utendaji kazi wa mtambo wa kusafisha maji kuwa safi na salama kwaajili ya kunywa walioutoa Kama msaada katika mahabusu ya watoto iliyopo Upanga Jijini Dar Es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya DAVIS & SHIRTLIFF, Bw Benjamin Munyao akimuonyesha Kamishna Wa Ustawi wa Jamii, Mh Dunford Makalla jinsi mtambo huo unavyofanya kazi ya kusafisha maji na kuwa salama na safi kwaajili ya Kunywa.
 Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya DAVIS & SHIRTLIFF na waandishi wa habari wakifuatilia hafla hiyo fupi.Picha na Josephat Lukaza

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni