Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amerejea nchini humo akitokea The Hague, Uholanzi ambako alifika katika mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ( ICC ) kusikiliza mashitaka yanayomkabili katika mahakama hiyo.
Rais Kenyatta akiwa ameongozana na mkewe, aliwasili katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta leo saa 12.30 asubuhi kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Kenya ( KQ ) na kupokelewa na Naibu wake, William Ruto ambaye alikuwa kaimu Rais.
Rais Kenyatta akifurahia jambo na Naibu wake William Ruto ambaye alikuwa Kaimu Rais.
Rais Uhuru Kenyatta akitazama ngoma mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa JKIA.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni