Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiangalia fuvu la aliyekuwa Chifu wa Wahehe, Mkwawa alipotembelea Makumbusho ya shujaa huyo aliyepambana na wajerumani na kujiua kwa bunduki baada ya kuona yupo hatarini kukamatwa na wajerumani.
Mrithi wa Chifu Mkwawa, Abdul Adam Mkwawa akimkaribisha Kinana kutembelea makumbusho ya Chifu Mkwawa katika Kijiji cha Kalenga, Iringa Vijijini wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010.
Zuberi Mwamitala akimuonesha Kinana maandishi ya kiarabu aliyowahi andika Chifu Mkwawa enzi za uhai wake.
Mwamitala akionesha kisanduku kilichokuwa kimehifadhi fuvu la Chifu Mkwawa nchini Ujerumani na hatimaye kurejeshwa nchini.
Mwamitala ambaye ni mtunza kumbukumbu katika makumbusho ya Mkwawa, akionesha baadhi ya mabomu yaliyotumiwa na askari wa kihehe waliopambana na wajerumani
Kinana akioneshwa madini ya chuma yaliyotumiwa enzi za Chifu Mkwawa kutengenezea silaha mbalimbali pamoja na shoka na majembe.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni