.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 7 Oktoba 2014

RAIS KENYATTA ASEMA ANAKWENDA KUSIKILIZA KESI INAYOMKABILI THE HAGUE, NCHI AMWACHIA MH RUTO

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema atakwenda katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu ( ICC ) iliyopo The Hague, Uholanzi. 

Pia rais Kenyatta ametangaza kuwa, akiwa nje ya nchi, Naibu wake Mh William Ruto ndiye atakaimu nafasi yake mpaka atakaporejea. 

Akilihutubia Bunge la Kenya hapo jana, Rais Kenyatta amesema kuwa yupo tayari kufika mbele ya mahakama hiyo ili ukweli na haki ipatikane.
Naibu Rais wa Kenya, William Ruto ( ndani ya gari ) atakaimu nafasi ya Urais kwa kipindi chote ambacho Rais Uhuru Kenyatta atakapokuwa katika mahakama ya ICC kusikiliza mashitaka yanayomkabili.
Zaidi ya watu 1,200 walipoteza maisha yao nchini Kenya kufuatia machafuko yaliyozuka baada ya uchaguzi mkuu wa Rais wa mwaka 2007.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni