Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akihutubia wakati wa hafla ya kutafuta uwezo wa Kununua Vitabu 2,500 vyenye thamani ya shilingi milioni 218, kwa ajili ya kusaidia shule 10 msingi na Sekondari za Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam ya Shirika Lisilo la Kiserikali lijulikanalo kama Nkwamira Sustainable Life Trust, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jana usiku Oktoba 10, 2014 jijini Dar es Salaam.
NHC imechangia kiasi cha shilingi milioni 12, na imeahidi kujenga madarasa mawili katika shule ya msingi Saku iliyopo Mbagala.
Azim Jamal ambaye ni mwanzilishi na mkurugenzi wa Corporate Sufi Worldwide Inc kampuni inayojishughulisha na kusaidia wadau na makampuni kupata stahiki katika kazi zao,na ni mwandishi wa vitabu mbalimbali vilivyotafsiriwa katika lugha 10, akizungumza katika hafla hiyo jana.
Mwenyekiti wa Bodi ya Madini nchini, Richard Kasesela akizungumza wakati wa hafla ya kutafuta uwezo wa Kununua Vitabu 2,500 vyenye thamani ya shilingi milioni 218, kwa ajili ya kusaidia shule 10 msingi na Sekondari za Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, ya Shirika Lisilo la Kiserikali lijulikanalo kama Nkwamira Sustainable Life Trust.
Wadau waliofika katika hafla hiyo jana katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mazungumzo ya wageni waliofika katika hafla hiyo.
Muongozaji wa sherehe hiyo maarufu kama MC Luvanda, Anthony Luvanda akiinua picha juu kuinadi kwenye hafla hiyo ya uchangiaji kwaajili ya kuwezesha watoto kupata vitabu vya kusoma.
Mgeni rasmi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akipokea hundi ya Shilingi milioni saba iliyotolewa na Benki ya KCB jana jioni.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akijadiliana jambo na Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai, Omari Mjenga kwenye hafla hiyo.
Wadau Abdul Njaidi na mwenzie wakifuatilia jambo katika hafla hiyo jana katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mazungumzo ya wageni waliofika katika hafla hiyo.
Wadau waliofika katika hafla hiyo jana katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mazungumzo ya wageni waliofika katika hafla hiyo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Saku wakitoa ushuhuda wao wa namna wanavyopata shida kupata elimu katika shule yao hiyo ambapo walisema wengi wao wanakaa chini na vitabu na madarasa hayatoshi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni