Mwenyekiti wa Bodi ya Madini nchini, Richard Kasesela ( kushoto ) akiwa na Mkurugenzi wa Radio One, Deogratius Rweyunga wakishiriki matembezi ya hisani yaliyoanzia Kanisa Katoliki Mwenge na kuishia Kanisa Katoliki - Sinza Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mwokozi. Matembezi hayo yaliongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh Bernad Membe.
Mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh Bernad Membe akiongea katika harambee ya kuchangia ujenzi wa ghorofa la Kanisa Katoliki - Sinza, Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi. Kulia kwake ni Paroko wa Parokia hiyo Cuthbert, Maganga.
Katika matembezi hayo yaliyokuwa na lengo la kukusanya zaidi ya shilingi milioni 200, fedha taslimu zaidi ya milioni 55 zilipatikana, huku Waziri Membe na marafiki zake wakiahidi kuchangia milioni 50, ambapo leo ametoa milioni 25 na nyingine 25 akiahidi kutoa ndani ya wiki mbili zijazo.
Pia Waziri Membe amemuahidi Paroko Maganga kuwatafuta wafadhili zaidi ili kukamilisha ujenzi wa ghorofa hilo.
Paroko wa Kanisa Katoliki Sinza, Parokia wa Bikia Maria Mama wa Mkombozi Cuthbert Maganga akimshukuru mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh Bernad Membe ( katikati ) kwa kukubali kushiriki matembezi hayo.
Waumini wakichukua picha za kumbukumbu za tukio hilo la kipekee.
Mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh Bernad Membe ( aktikati ) akiwa na Paroko wa Kanisa Katoliki - Sinza, Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mwokozi, Cuthbert Maganga ( mwenye vazi jeupe ) katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Kanisa hilo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni