Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini
Oscar Pistorius amerejea mahakamani tena hii leo katika siku ya pili
ya malumbano ya hukumu yake iwapo afungwe jela kwa kumuua mpenzi wake
Reeva Steenkamp.
Hapo jana Mwendesha Mashatka
alikasirishwa na afisa wa adhabu mbadala kuitaka mahakama impatie
kifungo cha nyumbani pamoja na kufanya kazi za kujitolea za jamii, na
kusema ombi hilo halikubaliki.
Mwezi uliopita mwanariadha huyo
alipatwa na hatia ya kumuua kwa kumpiga risasi mpenzi wake huyo bila
ya kukusudia, na kufutiwa shitaka la kuua kwa makusudi lililokuwa
likimkabili.
Pistorius anakabiliwa na kifungo
jela cha miaka 15, ingawa Jaji Thokozile Masipa anaweza kutotoa
adhabu hiyo na badala yake amtake alipe faini.
Oscar Pistorius akiingia mahakamani hii leo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni