Rais Uhuru Kenyatta amehairisha
ziara yake ya siku tatu katika kaunti ya Kisumu, iliyokuwa imepangwa
kuanza kesho baada ya kufanya mkutano na viongozi wa Nyanza Ikulu
Jijini Nairobi.
Katika taarifa iliyotolewa na
mshauri wa rais Bw. Joshua Kutuny, ziara hiyo imehairishwa hadi wiki
ijayo katika kutoa fursa ya maandalizi mazuri, ili ziara hiyo iwe ya
mafanikio katika kaunti hiyo ambayo ni ngome ya mpinzani wake mkuu
Bw. Raila Odinga.
Katika ziara hiyo, Rais Kenyatta
anatarajiwa kufungua miradi kadhaa huko Kisumu pamoja na kuongoza
kikao cha baraza la mawaziri.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni