Shirika la Afya Duniani (WHO)
limesema mlipuko wa Ebola unatishia uwepo wa jamii na unaweza
kupelekea kuanguka kwa mataifa.
Mkuu wa WHO, Margaret Chan amesema
mlipugo wa ugonjwa huo hatari ambao umeshaua watu 4,000 huko Afrika
Magharibi, umepelekea kuibua mgogoro wa amani na usalama wa
Kimataifa.
Bi. Chan ameonya kuwa gharama za
hofu za ugonjwa huo zinasambaa haraka kuliko hata virusi vya ugonjwa
huo.
Wakati huo huo madaktari wamepuuzia
mgomo ulioitishwa nchini Liberia, ambayo ndio kitovu kikuu cha
maambukizi hatari ya Ebola.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni