Waziri wa nchi anayehusika na
Maadili na Uadilifu, Simon Lokodo amelitaka jeshi la polisi kumhoji
mwanamuziki Desire Luzinda kutokana na picha zake za utupu
zinayodaiwa kupigwa na rafiki yake wa kiume Mnaigeria ambazo zimesambaa
kwenye mitandao ya jamii.
Akiongea na gazeti moja la nchini
humo, Waziri Lukodo amesema tayari ameliangiza jeshi la polisi
kuwakamata wahusika na kwa sasa jeshi hilo lipo mbioni kumkamata
Luzinda na rafiki yake huyo wa kiume.
Waziri huyo amesema Luzinda na
rafiki yake huyo wa kiume watashitakiwa kwa kuonyesha picha za utupu,
chini ya kifungu namba 13, cha Sheria ya kukukabiliana na picha za
ngono.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni