Mitch McConnell kuongoza Seneti
Chama cha Republican kimejiimarisha
zaidi katika Seneti kwenye uchaguzi wa muhula wa kati, na kujijenga
zaidi katika miaka ya mwisho kabla ya Rais Barack Obama hajamaliza
muda wake wa urais.
Kujimarisha huku kwa Republican
kumechangiwa na kupata ushindi katika majimbo ya Arkansas, Montana,
South Dakota, West Virginia na Colorado, North Carolina.
Kwa ushindi huo Mitch McConnell
atakuwa kiongozi wa baraza la Seneti, ambapo chama cha Republic pia
kinajipanga kuongeza wingi wao katika barala la wawakilishi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni