.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 28 Januari 2015

AFCON 2015, GHANA YASONGA MBELE ROBO FAINALI BAADA YA KUIFUNGA AFRIKA KUSINI 2-1

Timu ya soka ya taifa ya Ghana imefanikiwa kufuzu kwa hatua ya robo fainali ya michuano ya kuwania kombe la mataifa Afrika baada ya kuifunga Afrika Kusini " Bafana Bafana " kwa jumla ya magoli 2-1 katika mchezo wa kundi C hapo jana. 

Katika mchezo huo ilibidi Ghana wapambane kufa na kupona ili kuhakikisha wanasonga mbele baada ya kuwa wametangulia kufungwa bao katika dakika ya 17 ya kipindi cha kwanza na mchezaji mahiri wa Afrika Kusini, Masango. 

Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika. Kipindi cha pili ndipo Ghana walipofanikiwa kupata mabao hayo mawili katika dakika za 73 na 83 wafungaji wakiwa ni Boye na Andre Ayew. 

Kwa matokeo hayo Ghana imesonga mbele hatua ya robo fainali baada ya kumaliza ikiwa inaongoza kundi C kwa kuwa na pointi 6.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni