Hatua ya robo fainali ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika zinaanza kutimua vumbi kesho huko nchini Equatorial Guinea zinakofanyika fainali hizo.
Kesho timu za kwanza kushuka dimbani itakuwa kati ya Congo ambayo itamenyana na wenzao wa Congo DRC.
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo, utafuatia mchezo katika ya Tunisia ambao watacheza na wenyeji wa fainali hizo Equatorial Guinea, mchezo ambao unatarajiwa kuwa na upinzani mkali.
Siku ya jumapili kutakuwa na mechi nyingine za hatua hiyo ya robo fainali, ambapo Ghana watacheza na Guinea kisha kufauatiwa na mchezo kati ya Ivory Coast watakaomenyana na Algeria
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni