Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni mfuasi wa kundi la Boko Haram, amejilipua kwa bomu katika soko lililopo jimbo la Gombe nchini Nigeria.
Katika tukio hilo, jumla ya watu sita wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa.
Pamoja na kwamba mpaka sasa hakuna mtu au kikundi kilichosema kinahusika na tukio hilo, lakini kundi la Boko Haram linahusishwa kwa tukio hilo.
Tayari maelfu ya watu wamefariki dunia aidha kwa kupigwa risasi kwa mabomu tangu kundi hilo lianze kufanya uasi wake nchini Nigeria kwa miaka mitano.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni