Katika mchezo uliozikutanisha Ivory Coast na Mali, nchi hizo zilitoka uwanjani zikiwa zimefungana bao 1-1.
Mali ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa kunako dakika ya 6 na mchezaji Bakary Sako, bao ambalo lilidumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na ilionekana wazi jahazi la Ivory Coast lilikuwa linataka kuzama kutokana na kuelemewa na Mali.
Lakini katika dakika ya 86 ya mchezo, Max Gradel aliisawazishia Ivory Coast na kufanya matokeo kuwa 1-1.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni