Timu ya taifa ya Ghana jana ilikumbana na kipigo cha mabao 2-1 toka kwa Senegal katika mchezo wa kundi C wa michuano ya fainali za Mataifa ya Afrika zinazoendelea nchini Equatorial Guinea.
Pamoja na kutangulia kupata bao kwa njia ya penati katika dakika ya 14 ya mchezo kupitia kwa Andrew Ayew, Ghana walishindwa kulilinda bao hilo na kujikuta wakimaliza mchezo huku wakiwa wamefungwa mabao 2-1.
Mabao ya Senegal, maarufu kwa jina la Simba wa Teranga inayoonekana kuimarika sana katika fainali hizi yaliwekwa kimiani na wachezaji Biram Diofu katika dakika ya 58 na bao la pili nala ushindi likifungwa na Moussa Sow dakika ya 90 ya mchezo huo.
Kwa matokeo hayo, Algeria inaongoza kundi C ikiwa na pointi 3 sawa na Senegal lakini ikiwa na mabao zaidi, huku Ghana wakiwa nafasi ya tatu na Afrika Kusini wakiwa mkiani
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni