Mmoja wa Makamanda waandamizi wa
kundi la waasi la Lord's Resistance Army (LRA) la nchini Uganda,
Dominic Ongwen, ambaye amejisalimisha kwa majeshi ya Marekani
amewataka makamanda za zamani wa kundi hilo kujisalimisha na kutoka
msituni na kumaliza uasi.
Ongwen ambaye anakabiliwa na
mashitaka katika mahakama ya kimataifa ya makosa ya uhalifu ICC
alikamatwa wiki iliyopita nchini Afrika ya Kati (CAR) na kusema
kwamba pia amepokea msamaha kutoka kwa rais wa Uganda Yoweri Museveni
ingawa serikali ya Uganda haijasema lolote kuhusu kauli hiyo.
Kundi la LRA limekuwa likilaumiwa
kwa kuuwa watu zaidi ya 100,000 na kuteka watu zaidi ya 60,000 ikiwa
ni pamoja na watoto katika mapambano yaliyodumu kipindi cha miongo
mitatu katika nchi tano za Afrika ya Kati.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni