Kanisa katoliki jana limeshindwa
kujaribu kutafuta upatanishi wa mgogoro wa mishahara ya walimu
uliopelekea mgomo uliodumaza kabisa masomo katika shule zote za umma
nchini Kenya kwa wiki ya pili sasa tangu uanze.
Majadiliano hayo yaliyoongozwa na
Askofu Maurice Crowley, ambaye ni msimamizi wa Elimu wa Kanisa
Katoliki, yaliyofanyika Jijini Nairobi yalikuwa yakitarajiwa kumaliza
mgomo huo, ulioathiri shule za umma nchi nzima, yalikwama baada ya
viongozi wa vyama vya walimukutoka nje.
Walimu nchini Kenya walianza mgomo
wao, jumatatu iliyopita baada ya kudai mazungumzo yao na Tume ya
Huduma za Walimu yaliyoanza mwaka jana yamekwama.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni