Msemaji wa jeshi la Uganda amesema
kamanda mwandamizi wa waasi wa nchi hiyo wa Lord's Resistance Army
(LRA) atapelekwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita
(ICC).
Kamanda huyo Dominic Ongwen,
inaaminika kuwa ni kamanda msaidizi wa kiongozi wa waasi hao wa LRA
wanaoongozwa na Joseph Kony, anashikiliwa na wanajeshi wa Marekani
tangu wiki iliyopita, katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Kamanda Ongwen na kiongozi wake
Joseph Kony wanatafuta na mahakama ya ICC kwa makosa ya uhalifu dhidi
ya binadamu, kutokana na kusababisha mauaji ya watu, kuwashambulia,
kuwakata viuongo na kuwateka watoto na wanawake.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni