.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 19 Januari 2015

LA LIGA, REAL MADRID YAITANDIKA GETAFE, NAYO BARCELONA YAIVURUGA DEPORTIVO LA CORUNA HUKU MESSI NA RONALDO WAKIONGOZA MAUAJI

Mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo jana aliiongoza vyema timu yake ya Real Madrid kuitandika Getafe kwa jumla ya mabao 3-0 katika mchezo wa ligi kuu nchini Hispania " La Liga ". 

Katika mchezo huo ambao kipindi cha kwanza Getafe waliokuwa wakicheza uwanja wao wa nyumbani walionekana kuukamia na kufanya timu hizo kwenda mapumziko bila kufungana.

Ronaldo alifunga bao la kwanza katika dakika ya 63 na kisha akafunga bao la tatu katika dakika ya 79. Bao la pili la Real Madrid lilifungwa na Gareth Bale katika dakika ya 67.
Wachezaji wa Real Madrid, Ronaldo, Benzema na James wakipongezana baada ya Ronaldo kuifungia timu yake bao dhidi ya Getafe hapo jana.
Katika mchezo mwingine wa ligi kuu nchini Hispania hapo jana FC Barcelona waliitandika bila huruma moja kati ya timu kongwe nchininhumo, Deportivo La Coruna kwa jumla ya mabao 4-0 huku Lionel Messi akionyesha umahiri wake wa kucheka na nyavu.
Katika mchezo huo Messi aliifungia timu yake mabao matatu katika dakika za 10, 33 na 62 huku mchezaji wa Deportivo La Coruna, Sidnei akijifunga katika dakika ya 83 ya mchezo huo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni