Katika mchezo huo wa kundi B, Tunisia ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 70 mfungaji akiwa ni Ali Moncer.
Bao la kusawazisha la Cape Verde lilifungwa kwa mkwaju wa penati na Almeida Ramos katika dakika ya 77 ya mchezo huo.
Katika mchezo mwingine wa fainali hizo za kuwania kombe la Mataifa ya Afrika, Zambia nao walijikutwa wakibanwa na Congo DRC baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1.
Katika mchezo mwingine wa fainali hizo za kuwania kombe la Mataifa ya Afrika, Zambia nao walijikutwa wakibanwa na Congo DRC baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1.
Pamoja na kutangulia kupata bao katika dakika ya pili tu ya mchezo huo kupitia kwa mshambuliaji wake Given Singuluma, haikutosha kuwafanya Zambia waondoke na pointi zote tatu muhimu katika mchezo huo, kwani Congo DRC walisawazisha katika dakika ya 66 mfungaji akiwa ni Bolasie.
Huo ulikuwa mchezo mwingine wa kundi B ulioshuhudia sare ya bao 1-1.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni