.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 18 Januari 2015

LIGI KUU UINGEREZA, CHELSEA YAIFANYIA MAUAJI SWANSEA, MAN UNITED YANG'AA UGENINI DHIDI YA QPR, LIVERPOOL YAITAMBIA ASTON VILLA

Mabao matano yaliyofungwa kwa ufundi wa hali ya juu na wachezaji Oscar ( dakika ya 1 na 36 ), Diego Costa ( dakika za 19 na 34 ) na bao la tano lililofungwa na Andre Schurrle dakika ya 79 yalitosha kabisa Chelsea kuiangamiza Swansea waliokuwa wakicheza nyumbani. 

Katika mchezo huo wa ligi kuu nchini Uingereza, Chelsea walionekana tangu mwanzo wa mchezo kuwa wamepania kuibuka na ushindi mnono.
Kwa matokeo hayo, Chelsea wameendelea kujikita kileleni baada ya kufikisha pointi 52 wakizidi kuwakimbia mabingwa watetezi, Manchester City walio nafasi ya pili wakiwa na pointi 47.
Katika mchezo mwingine wa ligi kuu nchini Uingereza hapo jana, mashetani wekundu, Manchester United waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya QPR ambao walikuwa wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani. 

Mabao ya Man United yaliwekwa kambani na wachezaji 
Marouane Fellaini katika dakika ya 58 na bao la pili likifungwa na James Wilson katika dakika ya 90. 

Pamoja na ushindi huo, Manchester United wamesimama nafasi ya nne wakiwa na pointi 40 huku Southamton wakiwa nafasi ya tatu wakiwa na pointi 42.
Liverpool nayo jana ilifanikiwa kupata pointi tatu muhimu na kufikisha jumla ya pointi 35 wakiwa nafasi ya saba katika msimamo wa ligi kuu Uingereza baada ya kuifunga Aston Villa mabao 2-0. 

Aston Villa wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani, walishindwa kuwazuia Liverpool kuwafunga katika mchezo huo. 

Mabao ya Liverpool yalifungwa na Fabio Borini katika dakika ya 24 na bao la pili likifungwa na Rickie Lambert katika dakika ya 79. 

Matokeo ya michezo mingine ya ligi kuu Uingereza iliyochezwa jana ni kama ifuatavyo:- 

Newcastle 1 vs 2 Southampton

Tottenham 2 vs 1 Sunderland

Leicester 0 vs 1 Stoke

Burnley 2 vs 3 Crystal Palace

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni