.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 21 Januari 2015

MGOMO WA MAGARI MADOGO YA ABIRIA WALETA ADHA HUKU UKIGUBIKWA NA VURUGU




MAGARI madogo ya abiria katika jiji la Arusha maarufu kwa jina la vifodi, leo yamegoma kutoa huduma wakipinga kutumia utaratibu mpya wa njia ndefu na kuzua vurugu kubwa kati kati ya jiji, huku wananchi wengi wakitembea kwa miguu umbari mrefu.

Vurugu hizo, zimekuwa zikisababishwa na makundi ya vijana wapiga debe, kuvunja vioo vya magari ambayo yalikuwa yamekaidi msimamo wa mgomo na kusababisha askari wa FFU kuingilia kati kuwatawanya.

Mamia ya abiria, wakiwepo wanafunzi na wafanyabiashara, leo wamelazimika kutembelea kwa miguu na wengine kukodi pikipiki maarufu kama boda boda.

Katika barabara za Sokoine,Arusha- Babati ambapo magari ya Njiro- Stendi ndogo, Kwa mrombo- Samunge na Majengo- Kituo na Fire-Stendi ndogo Kijenge- mjini na maeneo mengine magari ambayo hufanya safari yalikuwa hayapo barabarani.

Mmoja wa madereva wa daladala, John Mathias amesema wanapinga kutumia njia ndefu, kwani stendi mpya ya Samunge haina vyoo na pia hakuna maeneo ya vituo vipya vilivyotengwa katika njia hizo na hata ikinyesha hakuna mahali pa kujificha kujikinga na mvua.

Kutokana na mgogoro huo, maafisa wa jiji la Arusha, chama cha wasafirishaji na Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majani (SUMATRA) wamekutana kwa dharura na baada ya kikao, waliazimia utaratibu mpya kuendelea.

Mhandisi wa Barabara wa Jiji la Arusha, Fordia Mwankenja na Afisa habari wa jiji la Arusha,Ntigenjwa Hosea wamesema utaratibu mpya utaendelea, sababu madai yao hayana ukweli pale kituo cha Samunge kuna choo tayari na pia vituo vimetengwa na vingine vitatengwa.



Jiji la Arusha litaanza rasmi kutekeleza maazimio ya wadau wa usafiri wa daladali kwa kuanzisha njia ndefu wenye lengo la kuondoa msongamano wa daladala katikati ya Jiji jana.



Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji na ni Diwani wa Kata ya Moshono, Paul Matthysen amesema utaratibu wa njia ndefu ndio suluhu ya msongamano wa magari kati kati ya jiji.



Makubaliano hayo, yameridhiwa na wasafirishaji, Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(Sumatra) ,Baraza la Huduma za Wasafiri (Sumatra CCC), Halmashauri ya Jiji la Arusha na polisi wa usalama barabarani.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni