.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 21 Januari 2015

KINANA KUWAPELEKA WAANDISHI WA HABARI SUDANI KUSINI KUJIONEA MADHARA YA VITA

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahamani Kinana, amesema mara baada ya kusaini mkataba wa kuacha mapigano Sudani Kusini, Tanzania inatarajia kuwapeleka waadishi wa habari wa vyombo mbalimbali nchini Sudan Kusini, ili kujifunza athari za vita
vilivyotokea kwa ajili ya kugombea madaraka.

Akizungumza leo Jijini Arusha, kabla ya kusaini makubaliano hayo, aliwaambia waandishi wa habari kuwa wajiandae kwenda Sudani Kusini ili wakajifunze athari za vita kwa ajili ya kuelimisha wananchi na viongozi.

Amesema katika kuonyesha kuwa amedhamiria kuwahakikisha waandishi wanapata uelewa wa kutosha katika kuandika na kutangaza madhara ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, Kinana ameahidi kuwa atahakikisha anawapeleka waandishi wa habari wa Arusha waitembelee Sudan Kusini.

Amesema anaamini watakapokwenda kujionea kwa macho madhara ya vita wataweza kutumia vema kalamu zao kuelimisha watanzania madhara ya vita.


Kinana alisema kwa kuwa wao kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) kiliombwa kufanya mazungumzo juu ya vita hiyo na ndivyo watakavyofanya pia kwa waandishi ili wapate somo,”alisema.

Amesema mapigano hayo uyamesababisha uchumi wan chi hiyo kurudi nyuma, ukizingatia kuwa wao ni wazalishaji wakubwa wa ng’ombea na watatu katika nchi za Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya mifugo.

Kinana amesema lakini kwa sababu ya vita idadi ya mifugo hiyo imepungua kwa kiasi kikubwa huku uchumi wan chi ukiyumba na kusababisha umaskini kwa wananachi.

amesema Sudan Kusini ilihangaika miaka zaidi ya 50 kutafuta uhuru wao, miaka miwili baada ya kujitenga kutoka Sudan Kaskazini, baada ya asilimia 90% kupiga kura ya kujitenga wakaanza vita ya kugombea madaraka, sasa kila familia imeathirika kutokana vita ndio wanasaka amani.

Mazungumzo ya kutafuta amani kwa nchi hiyo yalianza mapema Desemba 23 na 24 mwaka jana 2014 katika hotel ya Ngurudoto, Wilayani Arumeru, Mkoan Arusha, huku zikiwakutanisha pande zote tatu zinazopigana kwa ajili ya kusaka madaraka.

Katika mazungumzo hayo mwenyekiti wa mazungumzo hayo ni Balozi Dk. Samweli Malecela, ambaye pia alikuwa ni Waziri Mkuu Mstaafu awamu ya pili ya uongozi wa Rais Ally Hassan Mwinyi.

Mapigano hayo ya ndani ya chama cha SPLM katika nchi ya Sudani Kusini yanayohusish makundi matatu ambapo kila kundi linataka madaraka ya kuongoza nchi hiyo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni