Mwanaume mmoja aliyekuwa na bastola
feki, amekamatwa baada ya kuvamia studio za kituo cha televisheni ya
taifa ya Uholanzi ya NOS, na kupelekea taarifa ya habari ya usiku
kutorushwa.
Mwanaume huyo aliyevalia vizuri
akiwa ameshika mkononi bastola hiyo refu yenye kiwambo cha kuzuia
sauti, alifanikiwa kupenya na kuingia studio, na kushinikiza apewe
muda wa kuongea hewani.
Kufuatia tukio hilo kituo hicho cha
TV cha NOS, kililazimika kuzima matangazo yake kwa muda wa saa moja,
lakini kamera ziliendelea kumrekodi mwanaume huyo hadi pale polisi
walipofika na kumkamata.
Mtu huyo akiwa amenyanyua mikono baada ya polisi kuingia studio
Polisi wenye silaha wakimsogelea mtu huyo
Polisi wakimkandamiza chini ya sakafu mtu huyo ili kumfunga pingu




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni