.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 30 Januari 2015

WAPIGANAJI WAUWA WATU 26 NCHINI MISRI WAKIWEMO WANAJESHI

Watu wapatao 26 wamekufa katika mashambulio ya mfululizo yaliyofanywa na wapiganaji kaskazini mwa Penusula ya Sinai nchini Misri.

Bomu lililotegwa kwenye gari pamoja na kombora lililolenga wanajeshi, kaskazini mwa Sinai mji mkuu wa El-Arish limeuwa idadi kadhaa ya wanajeshi.

Mashambulio mengine yametokea karibu na mji wa Sheik Zuwayid na katika mji wa Rafah, unaopakana na Gaza.

Kundi la wapiganaji la Ansar Beit al-Maqdis, ambalo linaushirikiano na kundi la Dola ya Kiislam (IS) limesema limetekeleza mashambulio hayo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni