.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 29 Januari 2015

MWANASAYANSI ALIYETAKA KUUZA SIRI ZA NYUKLIA AFUNGWA MIAKA MITANO

Aliyekuwa mwanasayansi katika maabara ya taifa ya Los Alamos ya Marekani amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kujaribu kutoa siri za kutengeneza bomu la nyuklia kwa nchi za Venezuela.

Mwanasayansi huyo Pedro Leonardo Mascheroni, alikiri kosa hilo mnamo mwaka 2013, la kutoa siri kwa jasusi wa shirika la ujasusi la Marekani la FBI, ambaye alijifanya kuwa ni afisa kutoka Venezuela.

Pedro Mascheroni, mwenye umri wa miaka 79, anayetokea nchini Argentina, pia mkewe alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni