Kiongozi wa Australia Tonny Abbot
amesema mgomo wa kutokula wa wahamiaji katika eneo wanaloshikilia
umemalizwa.
Kauli yake imekuja baada ya walinzi
katika kambi ya kisiwa cha Manus Papua New Guinea, kuingia kwa nguvu
katika eneo ambalo wahamiaji hao walikuwa wanashikiliwa ambalo
waliamua kujizungushia uzio.
Baadhi ya wahamiaji hao imeripotiwa
kuwa wamekamatwa katika operesheni hiyo, ambayo imekuja baada mgomo
huo uliodumu kwa wiki moja. Hata hivyo wanaharakati wamedai baadhi ya
wahamiaji bado wanaendelea na mgomo wa kutokula.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni