.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 20 Januari 2015

POLISI WA IS WAWACHAPA BAKORA 90 WANAMUZIKI KWA KUTUMIA KIFAA CHA PIANO


Polisi wa Dola ya Kiislam (IS) wamepigwa picha za video wakiwachapa bakora wanamuziki na kuteketeza vifaa vyao vya muziki kama adhabu baada ya kubainika kupiga kifaa cha piano ambacho wanadai hakiendani na Uislam.

Watu hao wanaume wamepigwa picha wakichapwa bakora migongoni na miguuni katika eneo la wazi ili umma uone namna IS inavyotekeleza kwa vitendo sheria kali za kuzuia vifaa vya muziki vya kimagharibi.

Katika picha nyingine inaonekana piano pamoja na kifaa kingine cha muziki vikiwa vimeahribiwa kwa kupondwa pondwa katika eneo la Bujaq maili chache mashariki mwa Aleppo in Syria.
                        Mmoja wa wanamuziki hao akipigwa bakora za chini ya makalio
                                    Vifaa vya muziki walivyokutwa navyo kabla ya kuharibiwa 
                                                               Kwisha kazi kila kitu kimeteketezwa

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni