Papa Francis anaelekea nchini
Ufilipino kwa ajili ya ziara ya siku tano ambayo inangojewa kwa hamu
na taifa hilo lenye waumini milioni 80 wa Kanisa Katoliki.
Katika ziara hiyo jambo kuu
linalongojea ni mkusanyiko mkubwa wa watu katika misa ya wazi,
itakayofanyika katika Jiji la Manila siku ya jumapili.
Pia Papa Francis ataenda eneo la
Tacloban kukutana watu walionusurika na kimbunga kilicholeta maafa
mwezi Novemba mwaka juzi.
Ulinzi mkali umeimarishwa baada ya
majaribio mawili yaliyoshindwa ya kutaka kuwauwa mapapa waliopita.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni