.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 15 Januari 2015

MAHAKAMA YA KAZI YAFANIKISHAKUMALIZA MGOMO WA WALIMU KENYA

Vyama vikuu viwili vya walimu nchini Kenya jana vimekubaliana kumaliza mgomo wa walimu ulioingia wiki ya pili jumatatu ya wiki hii.

Chama cha Taifa cha Walimu Kenya (KNUT) na Chama cha Walimu wa Sekondari na Vyuo vya Ufundi (Kuppet) vimekubali kusitisha mgomo ili walimu warejee madarasani jumatatu ya wiki ijayo.

Makubaliano yamefikiwa mbele ya Jaji wa Mahakama ya Kazi, Nduma Nderi baada ya majadiliano yaliyofanyika mahakamani, yaliyohusisha vyama hivyo viwili na taasisi za serikali ya Kenya.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni