Papa Francis ametoa wito kwa
viongozi wa mataifa kukabiliana na rushwa na kumaliza tatizo la
kutokuwepo kwa usawa katika jamii, katika siku yake ya kwanza ya
ziara yake nchini Ufilipino.
Papa ametoa kauli hiyo alipokuwa
akizungumza wakati wa sherehe ya kumkaribisha nchini humo, katika
Ikulu ya Ufilipino na rais Benigno Aquino.
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki
Duniani jana alipokelewa na umati mkubwa wa waumini wa kanisa hilo
ambao ndio wengi zaidi nchini Ufilipino.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni