Rais Barck Obama wa Marekani,
amehudhuria gwaride la siku ya Uhuru wa India, Jijini Delhi, na kuwa
rais wa kwanza wa Marekani kufanya hivyo.
Rais Obama leo alikuwa ni mgeni
rasmi katika gwaride la mwaka la jeshi, ambapo aliwasili jana nchini
humo kwa ziara ya siku tatu ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi
hizo mbili.
Baada ya mazungumzo ya siku ya
jumapili, pande zote mbili zilitangaza kufikia makubaliano
yatakayoruhusu kampuni za Marekani kuiuzia India teknolojia ya
nyuklia kwa matumizi ya kiraia.



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni