Watoto wawili wakiume wa aliyekuwa
rais wa Misri, Hosni Mubarak wameachiwa kutoka jela siku moja baada
kufanyika kumbukumbu za vuguvugu ya nguvu ya umma iliyomg'oa
madarakani rais huyo.
Watoto hao Alaa na Gamal Mubarak
walitoka katika gereza la Torah leo Jijini Cairo na kuelekea nyumbani
kwao katika kitongoji cha Heliopolis.
Wiki iliyopita Mahakama iliagiza
watoto hao wa Mubarak, kuachiwa huru wakingojea shauri la tuhuma za
rushwa pamoja na baba yao.
Mahakama ilitoa uamuzi watoto hao
wameshakaa kizuizini katika muda mrefu kabla ya kusikilizwa kwa kesi
hiyo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni