Rais Barck Obama ametangaza kuisha
kwa mgogoro wa uchumi, na kuahidi sera za kiuchumi zitakazowanufaisha
Wamarekani wote.
Akitoa hotuba yake ya mwaka kwa
taifa kupitia baraza la Congress, ambayo ililenga wafanyakazi rais
Obama alielezea mikakati yake ya kuliinua kundi la uchumi wa kati.
Hata hivyo mikakati ya rais Obama
itakabiliwa na vikwazo na huenda isipitishwe kwenye baraza la
Congress linaloongozwa na wingi wa wajumbe kutoka chama cha
Republican.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni