.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 26 Januari 2015

SHIRIKA LA AFYA DUNIA (WHO) LIMEANDAA MPANGO WA KUJIFANYIA MABADILIKO

Shirika la Afya Dunia (WHO) limeandaa mpango wa kujifanyia mabadiliko, kwa kukiri kuwa lilichelewa mno kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola Afrika Magharibi.

Katika mkutano wa dharura Jijini Geneva, Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Margaret Chan amesema mlipuko huo wa Ebola, umeifundisha dunia namna inapaswa kuwajibika katika siku za baadae.

Zaidi ya watu 8,500 wamekufa kwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, wengi wao wakiwa ni wa nchini Sierra Leone, Guinea pamoja na Liberia.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni