Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita kwenye kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Kifaa kipya ndani ya Skylight Band John Music akiimba kwa hisia kaliii huku akipewa sapoti na Wenzake wa kwanza kushoto ni Baby na wa pili kutoka kushoto ni Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK47 na kulia ni Jessie.
Wanaume wa shoka wa Skylight Band kutoka kushoto ni Joniko Flower, Sony Masamba na Sam Mapenzi wakionyesha mbwembwe zao za kulisakata sebene kwa mashabiki wao, ambapo jioni ya leo watakuwepo kama kawaida kwenye kiota cha maraha Thai Village.
Mashabiki wa Skylight Band wakiburudika na muziki safi kabisa wa ladha na vionjo vya kila aina ikiwemo Reggae, Kwaito, Naija Flava, R&B, Zouk na zingine kibao bila kusahau sebene pale kati Joniko Flower anahusika sana sambamba na Sony Masamba.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni