Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick katikati akikata Utepe kama ishara ya Uzinduzi wa tawi Jipya la Uchumi Supermarket lililoko Mbezi Kawe karibu na ukumbi wa rainbow-mbezi chini jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa Uchumi SuperMarket (Afrika mashariki) Bw.Jonathan Ciano na Kulia ni Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik na Mkurugenzi mkuu wa Uchumi Supermarket(Afrika mashariki) Bw. Jonathan Ciano na Meneja wa Uchumi Supermark tawi la Mbezi Kawe, Bw. Evans Munga wakikata keki baada ya Uzinduzi wa tawi jipya.
Mkurugenzi Mkuu wa Uchumi SuperMarket (Afrika mashariki), Jonathan Ciano (kulia) akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik katika ufunguzi wa Tawi jipya la Uchumi lililoko Mbezi Kawe karibu na ukumbi wa Rainbow jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Said Meck Sadick akizungumza na wasambazaji na Wafanyakazi wa Uchumi Supermarket wakati wa Uzinduzi wa Tawi Jipya la Duka hilo.
Mbunge wa Nyamagana Mwanza Ezekiel Wenje, katikati akichagua moja ya Tiketi katika Shindano la kumtafuta mshindi wa shindano lijulikanalo kama ” Mimi Mwana Hisa “ kulia ni mkaguzi mwandamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha Emanuel Ndaki , na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Uchumi Supermarket (Afrika mashariki), Bw. Jonathan Ciano.
Mbunge wa Nyamagana Mwanza, Ezekiel Wenje katikati akinyosha juu moja ya Tiketi katika Shindano la kumtafuta mshindi wa shindano lijulikanalo kama ” Mimi Mwana Hisa “ kulia ni mkaguzi mwandamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha, Emanuel Ndaki na kushoto ni mkurugenzi wa Uchumi Supermarket,(Afrika mashariki) Jonathan Ciano na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadick, ambapo Elizabeth Robert ameibuka Mshindi wa Shindano hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Uchumi Supermarket,(Afrika mashariki) Bw.Jonathan Ciano (kushoto) akiweka Saini kwenye mfano wa hundi yenye thamani ya Tsh Milioni Tano, baada ya mkazi wa kinondoni kujishindia kiasi hicho katika Shindano lililoendeshwa na kampuni hiyo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni