Rais Barack Obama wa Marekani
amewasili nchini India kwa ziara ya siku tatu ambapo atalindwa na
ulinzi mkali ambao haujawahi kutokea.
Maelfu ya maafisa usalama wamewekwa
Jijini Delhi, pamoja na kufungwa kamera za ulinzi 15,000, vizuwizi
vya barabarani, pamoja na viroba vya kinga vilivyojazwa michanga.
Rais Obama atakuwa ni mgeni rasmi
hapo kesho katika maadhimisho ya Sherehe za Jamhuri ya India.
Baadae leo atafanya mazungumzo na
Waziri Mkuu Narendra Modi pamoja na kukutana na viongozi wa
wafanyabiashara.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni