Mchezaji nyota wa Real Madrid
Cristiano Ronaldo amejikuta matatani baada ya kugeuza mchezo wa soka
kuwa wa ngumi na mateke hapo jana kwa kumpiga mchezaji Edimar katika
mchezo wa La Liga.
Hii ni mara ya kumi kwa mwanasoko
huyo bora wa mwaka wa dunia kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika
maisha yake ya soko la kimataifa.
Ronaldo aliyeonekana kukereka
alitenda kosa hilo dakika ya 83, wakati Real na Cordoba zikiwa sare
ya bao 1-1, hata hivyo Gareth Bale alifunga bao katika dakika za
mwisho na kuipatia Real ushindi.
Baada ya tukio hilo, Ronaldo
alitwitti katika twitta yake maneno yasemayo anaomba msamaha kwa kila
mtu na hususan kwa Edimar kwa kitendo kisichofikirika alichokifanya
katika mchezo huo.
Cristano Ronaldo alipogeuka Bruce Lee kwa kumpiga ngumi pia Jose Angel Crespo
Edimar akianguka chini baada ya kupigwa teke na Cristiano Ronaldo
Cristiano Ronaldo akilambwa kadi nyekundu na refa




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni