Timu zinazowasili kwa ajili ya
michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Equatorial Guinea
zimekuwa zinatafuta malazi kutokana na kutokuwepo kwa vyumba vya
kutosha vya hoteli.
Kocha wa timu ya taifa ya Congo,
Claude Le Roy amesema wachezaji wake watano kati ya 35 hawajapata
vyumba vya kulala.
Le Roy amebainisha kuwa wachezaji
wengine wa timu yake wanalala kwenye hoteli zisizo na maji, na zenye
nywaya za umeme zilizowazi.
Kocha wa Burkina Faso, Paul Put pia
amekosoa miundombinu ya malazi ya nchi hiyo mwenyeji wa michuano ya
kombe la Mataifa ya Afrika na kusema michuano hiyo ingepaswa
kuhairishwa hadi mwezi Juni.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni