Ushahidi mpya unaonyesha wanawake
wanaotumia vidonge vya mpango wa uzazi aina ya Depo Provera, wapo
katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya Ukimwi, na kuzidi
kuungana na matokeo ya utafiti uliofanyika miaka minne iliyopita
kuhusu dawa hiyo.
Watafiti kutoka Taasisi ya Utafiti
wa Dawa Kenya (Kemri), Marekani na Sweden wamesema wanawake
wanaotumia dawa ya mpango wa uzazi ya Depo Provera wapo katika hatari
kubwa ya kupata maambukizi ya Ukimwi.
Timu ya watafiti huo, imefanya
uchunguzi kwa wanawake 228 Jijini Nairobi, baadhi yao wakitumia dawa
ya Depo Provera pamoja na dawa zingine za mpango wa uzazi, ambapo
wanawake waliotumia Depo Provera walikuwa na maambukizi zaidi ya
Ukimwi ikilingani na waliotumia dawa nyingine.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni