Jaji mmoja katika mji wa kusini mwa
Hispania, Granada, amewafungulia mashtaka mapadri 10, na wasaidizi
wao wawili wa Kanisa la Katoliki, kwa makosa ya kuwadhalilisha
kingono watoto.
Watuhumiwa hao 12 waliwadhalilisha
kingono watoto 4, kati ya miaka 2004 na 2007, uhalifu ambao
waliutekeleza katika nyumba ambayo ilikuwa ikitumika na mapadri.
Novemba mwaka jana Kiongozi wa
Kanisa Katoliki Papa Francis, alimpigia simu mmoja wa watoto
aliofanyiwa ukatili huo, ambaye sasa anaumri wa miaka 24, na kumuomba
msamaha kwa kitendo alichofanyiwa.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni