Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mathias Chikawe (kulia) akimuapisha Afisa wa Jeshi la Magereza, Elmas
Linus Mgimwa kuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Jeshi la Polisi
na Magereza inayoshughulikia masuala ya Utumishi na Utendaji wa
askari wa majeshi hayo, katika Ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es
Salaam leo. Kulia kwa Waziri Chikawe ni Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, na katikati ni Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mathias Chikawe (kulia) akimpa hati ya kiapo Afisa Utumishi wa wizara
hiyo, Ernest Maalugu kuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Jeshi la
Polisi na Magereza inayoshughulikia masuala ya Utumishi na Utendaji
wa askari wa majeshi hayo, katika Ukumbi wa Wizara hiyo jijini Dar es
Salaam leo. Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira
Ame Silima, na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak
Abdulwakil.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mathias Chikawe (kulia-meza kuu) akiongoza kikao cha Tume ya Jeshi la
Polisi na Magereza inayoshughulikia masuala ya kiutumishi na
kiutendaji wa askari katika Majeshi hayo, katika Ukumbi wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto Meza Kuu ni
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Picha zote na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni