Mkuu wa sera za Nje wa Umoja wa
Ulaya ametoa wito wa kuwepo kwa muungano mkubwa wa kukabiliana na
ugaidi utakaohusisha mataifa ya Kiislam.
Akiongea katika mkutano wa mawaziri
wa Umoja wa Ulaya Mkuu huyo Federica Mogherini amesema kunahaja ya
ushirikiano zaidi na mataifa ya Kiislam pamoja na ndani ya Umoja wa
Ulaya.
Mkutano huo umeitishwa kufuatia
tukio la kuuwawa watu 17 Jijini Paris pamoja na operesheni ya
kukabiliana na ugaidi nchini Ubelgiji.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni