Afya ya mtoto wa staa wa muziki
Bobby Brown, Bobbi Kristina imeripotiwa kutokuwa na mabadiliko
yoyote, taarifa inayokingana na ripoti zinazoendelea kusambaa kuwa
baadhi ya viungo vyake vimeanza kuacha kufanya kazi na kuhatarisha
zaidi uwezekano wa yeye kuendelea kuishi.
Chanzo cha karibu kabisa kutoka
familia ya binti huyo kimeeleza kuwa, kumekuwa na changamoto kubwa ya
kuibuka kwa habari za kupotosha kuhusu afya ya Bobbi Kristina, hali
yake ikiwa haina mabadiliko yoyote huku familia ikiendelea kuwa
karibu naye na matumaini ya kuimarika kwa afya yake yakiwa pale pale.
Bobbi Kristina ameendelea kupumua
kwa msaada wa mashine tangu alipopatikana akiwa hajitambui katika
sinki ya bafu nyumbani kwake Januari 31 mwaka huu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni