Misri imesema imeshambulia maeneo ya
kundi la Dola ya Kiislam (IS) nchini Libya, ikiwa ni saa chache tu
kupita baada ya kutokea tukio la kukatwa vichwa raia wake 21
Wakristo.
Televisheni ya taifa ya Misri,
imesema mashambulizi hayo yamelenga kambi, maeneo ya mafunzo na
maeneo ya kuhifadhi silaha ya kundi hilo.
Mapema rais Abdel Fattah al-Sisi
amesema Misri inahaki ya kujibu mapigo dhidi ya mauaji ya raia wake
yaliyofanywa na kundi la IS nchini Libya.
Ndugu wa raia wa Misri waliouwawa wakiandamana kuonyesha hasira zao
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni